Diamond Platnumz

Adam Nditi: Mimi sio hater, ni shabiki wa Diamond lakini show yake Uingereza haikuwa na standard niliyotegemea

Mchezaji wa klabu ya Chelsea ya nchini Uingereza, Adam Nditi amesema watu wasimwone kama ni hater baada ya kukosoa show ya Diamond nchini humo.

Adam Nditi of Chelsea

Kupitia Twitter, jana Adam alisema show ya Diamond ilikuwa mbovu nay a kutia aibu.

“Kwa wale wanaoniita hater kwa sababu ya tweet zangu kuhusu shoo ya Diamond juzi mimi namkubali sana Diamond na ni mshabiki wake mkubwa,” ametweet.

“Nazipenda nyimbo zake zote nazisikiliza karubuni kila siku ila juzi nilikuwa disappointed kwa sababu nilikuwa na matumaini makubwa ya shoo, ila ilikuwa haiko kwenye standard ambayo nilitegemea mmoja wa wasanii wakubwa wa Bongo kufanya.”

“Sasa jamani nadhani tunaelewana ukiniona hater endelea kuniita hater kama kuna kitu sikipendi ntasema sinyamazi,” amesisitiza mchezaji huyo mtanzania aliyechukua uraia wa Uingereza.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents