Michezo

Adebayor atemwa kwenye kikosi cha Tottenham

Emmanuel Adebayor ameachwa kwenye kikosi cha Tottenham Hotspur chenye wachezaji 25 kwaajili ya Premier League.

Manchester United v Tottenham Hotspur - Premier League

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 31 alitarajiwa kuondoka White Hart Lane lakini hakuna klabu iliyofikia makubaliano ya gharama za kumchukua.

Kutokana na hilo mchezaji huyo wa Togo ataendelea kupiga benchi Spurs hadi January pale ambapo atakuwa akifanya mazoezi na wachezaji wa ziada na timu ya vijana.

West Ham waliaminika kuwa mbioni kumsainisha kwa mkopo lakini walikuwa wameshafikia kikomo cha kuchukua wachezaji wa mkopo.

Hata hivyo mashabiki wengi wa Spurs wamekosoa uamuzi huo wakiamini kuwa ni bora angewekwa kwenye kikosi hicho hata kama angekuwa mchezaji wa ziada.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents