Michezo

Aden Rage awatahadharisha Watanzania ‘Hakuna mwanya wa Mtibwa Sugar kuwakilisha nchi’

Aliyekuwa Mwenyekiti wa klabu ya Simba, Ismail Aden Rage amewatahadharisha Mtibwa Sugar na Watanzania kuwa upo uwezekano mkubwa timu hiyo isipate nafasi ya kushiriki michuano ya Kombe la Shirikisho Barani Afrika CAF.

Rage ameyasema hayo kupitia kipindi cha michezo cha radio ya Magic FM, kufuatia klabu hiyo kupata adhabu kutoka Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika CAF mwaka 2000 kutoshiriki michuano wanayo iyandaa baada ya kushindwa kuwakilisha timu yao baada ya kukumbwa na ukata wa kifedha.

Kwanza nichukue nafasi hii kuwapongeza Mtibwa Sugar kwa ushindi waliyopata na kuonyesha jitihada kubwa kwenye mchezo wao na kufanikiwa kutawazwa kuwa mabingwa wapya wa Kombe la Shirikisho la Azam.

Nilitaka kuwatahadharisha Mtibwa na Watanzania kunauwezekano mkubwa wasipate nafasi ya kushiriki kwenye mashindano haya ya CAF, yeye ni bingwa wa michuano ya FA  barua waliyoandikiwa miaka 12 iliyopita bado haija futwa.

Kwa hiyo adhabu yao ya kufungiwa miaka miwili ya kutoshiriki mashindano yanayo andaliwa na CAF, Mtibwa hawajatekeleza.

Kwa sababu tangu Mtibwa Sugar wamefungiwa hawajawahi kushinda ligi au mabingwa wa FA Cup ili kupata fursa ya kushiriki kitu pekee ambacho Mtibwa wataweza kushiriki ni kama CAF imewasamehe nalo hilo halija tangazwa.

Hivyo sioni mwanya wa Mtibwa kuwakilisha nchi upo wapi, Mtibwa waliadhibiwa na Shirikisho la kandanda Afrika na sio TFF.

TFF ipo chini ya CAF sasa adhabu waliyopewa Mtibwa ni kutoshiriki mashindano yaliyoandaliwa na CAF na kwakipindi chote hicho hawakuwahi kuomba radhi vinginevyo kutoke msamaha kutoka Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika.

TFF yafafanua hatma ya Mtibwa Sugar kushiriki michuano ya CAF

Hata hivyo Rage amesema kuwa kutokuwa na maandalizi mazuri kwenye michuano ya kimataifa ndiyo imekuwa sababu kubwa ya Klabu za Tanzania kushindwa kufanya vizuri.

Hata hivyo Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini TFF kupitia kwa afisa habari wake, Clifford Mario Ndimbo wiki iliyopita alisema kuwa klabu ya Mtibwa Sugar inayo nafasi ya kushiriki mashindano hayo yanayo andaliwa na CAF.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents