Adidas yamtengenezea Mo Salah kiatu maalum (+Picha)

Nyota wa Liverpool, Mohamed Salah anatarajia kuvaa kiatu maalum kilichotengenezwa kwaajili yake kutoka katika kampuni ya Adidas kwenye mchezo wa Champions League baada ya kufanikiwa kufunga jumla ya magoli 100 siku ya Jumamosi mbele ya Everton.

Salah anakuwa mtu wa kwanza kufikisha idadi hiyo ya magoli Liverpool tangu mara ya mwisho kufanywa hivyo na Steven Gerrard mwaka 2008.

Mmisri huyo anakuwa nafasi ya tatu kwenye orodha ya wachezaji 17 wa Liverpool waliyofikia idadi hiyo ya magoli kutokana na idadi ya michezo aliyocheza, wakwanza akiwa Roger Hunt (akicheza michezo 144) wapili Jack Parkinson (153) na watatu ni Salah akifikisha idadi hiyo ya magoli kwenye michezo yake 159 aliyocheza.

Katika kusherehekea idadi hiyo ya magoli Adidas amemtengenezea kiatu maalum mchezaji huyo kutoka Afrika ambacho atakivaa siku ya Jumatano kwenye mechi yao ya Champions League dhidi ya Ajax.

Related Articles

Back to top button
Close
Bongo5

FREE
VIEW