Burudani

Afande atoa waraka kwa Ant Virus

AfandeSele
Mwanamuziki wa kizazi kipya Afande Sele, amelalamika juu wanamuziki wanaojiita wanaharakati  wa hapa nchini, ambao wanajiitaa Vinega  kwa kumtema  katika show ya uzinduzi wa albamu ya Ant Virus ambao itafanyika siku ya tarahe 26 kwenye viwanja vya Kijitonyama Posta.

 

Afande anasema  anajua wenzake wamemtenga kutokana na yeye kutajwa kuwa miongoni mwa wasanii watakao tumbuiza katika tamasha la Streit Music  Enter College Special, ambayo imeandaliwa na Clouse Fm.

Anasema yeye kukubali kujiunga na tamasha hilo kutokana na hali ya maisha yake, kwakuwa amegewa fedha nyingi na yeye anamatatizo na ndiyo maana amekubali kufanya show hiyo, ili kumaliza matatizo ya kifamilia. anasema wa  wanaharakati wenzake kufanya uzinduzi huo wa Ant Virus, kumtoza kunamamuuma sana kwa kuwa umuhimu wake ni mkubwa na amepanga nao mengi.

Ameendelea kusema watanzania wengi ndiyo mashahidi wa kauli yake na vitendo vyake juu ya harakati za muziki, pia anasema anasikitika sana kwamba Wanyonge kumtenga na kumsingizia Mwenzao mambo ambayo si ya kweli, ingawa wao ni mashahidi juu ya miongoni mwa watu waliobaniwa katika muziki.

Aidha amedai kwamba kitendo walichomfanyia kwenye mtandao wa Face Book kwamba si kizuri kwa kumtangazia kwamba amesanda, kushiriki katika show  hiyo wakati hawakumpa mwaliko, jambo ambalo anahisi kama ni kumdhulumu na kumyanyasa kwa hao ndugu zake, ambao anahisi kama vile wameanza kulewa kutoka na mafanikio madogo yanayotoka kwa Umma, ambao yeye amechangia kwa kiasi kikubwa sana.

Anasema yeye haumizwi sana kutengwa kwenye uzinduzi huo kwakuwa ni maamuzi yao. anasema Soggy Dog alimpa taarifa juu ya mchongo hiyo Show, na kumwambia kwamba atampa taarifa zote jambo ambalo alilipokea kwa furaha, huku akiwaaambia yupo tayari kwa kazi hiyo lakini hatmaye hakupewa tena taarifa yoyote, na matokeo yake anakutaka na matangazo ambayo yanamajina na jina lake halipo, na alipouliza hakupewa jibu zaidi ya kuzungushwa.

Afande anasema anatoa angalizo kwamba kwamba mambo haya yasichukuliwe kisiasa, pia kwa wadau na wanaharakati wa muziki kwamba ndiyo kwanza harakati ndiyo zimeanzishwa na kwamba wasibaguane, na wala kusingiziana kwakuwa wanadhalilishana, kwakuwa hawatakuwa wanafanya vyena kwa wanaadam na hata kwa Mungu.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents