Michezo

AFCON219: Je hili ndiyo kundi gumu kuliko yote  ?, ratiba nzima ya michuano hiyo hii hapa fainali kubwa Julai 19

Wakati zimesalia siku mbili pekee kabla ya kuanza kwa michuano ya Mataifa ya Afrika nchini Misri  Afcon 2019, kumwkuwa na maswali hasa kuwa lipi ni kundi la kifo ama gumu kati ya sita yaliyopo.

Image result for taifa stars vs misri

Kwa mashabiki wa soka upande wa Afrika Mashariki, kundi lilolomo midomoni mwao zaidi ni C, na wengi yamkini wakilitazama kundi hilo kama gumu zaidi kwenye michuano hiyo. Kundi hilo linaundwa na timu jirani na hasimu za Tanzania na Kenya pamoja na timu zenye uzoefu na wachezaji wakubwa kimataifa za Senegal na Algeria.

Lakini je, kundi hilo ni gumu kiuhalisia ama ni hisia tu za wapenzi wa kandanda wa Kenya na Tanzania?. Kwa wafuatiliaji wa kandanda na wachambuzi, kundi hilo linaonekana kuwa ni la kawaida, huku Senegal yenye wachezaji wakubwa kama Sadio Mane na Khalidou Koulibaly na Algeria zikipigiwa upatu kusonga mbele.

Iwapo Tanzania na Kenya itaifunga timu yoyote kati ya hizo matokeo hayo yatachukuliwa kama ya kushangaza kwenye ulimwengu wa kandanda.

Kama kundi C siyo gumu, basi kundi lipi ni gumu ama la kifo kama ifahamikavyo kwenye lugha za kimichezo?

https://www.instagram.com/p/BwKwB39juC7/

Wachambuzi wanaamini kuwa kundi D lenye timu za Ivory Coast, Morocco, Afrika Kusini na Namibia.

Timu tatu katika hizo ukiacha Namibia washawahi kunyakua ubingwa wa Afcon hapo kabla. Na ukiangalia uhalisia timu ya Namibia haipigiwi upatu kupenya kwenye kundi hilo.

Swali ni timu zipi mbili katika mabingwa hao wa zamani watafuzu kwa hatua ya mtoano ya michuano hiyo?

Kwa mujibu wa takwimu za ubora wa timu zinazotolewa na Shirikisho la Soka Ulimwenguni Fifa, Morocco ndiyo timu yenye kiwango cha juu zaidi kwenye kundi hilo ikishika nafasi ya 47 duniani, ikifuatiwa na Ivory Coast katika nafasi ya 62, Afrika Kusini nafasi ya 72 huku Angola ikiachwa mbali katika nafasi ya 113.Samatta

Haki miliki ya Je Mbwana Samatta atawika mbele ya Senegal na Algeria ?

Ni vyema kuwa na tahadhari lakini kuwa, si mara zote takwimu za nje ya uwanja huwa na uhalisia uwanjani.

Mwaka 2012, timu ya taifa ya Zambia ambayo haikuwa wachezaji wenye majina makubwa iliushangaza ulimwengu wa kandanda kwa kuchukua kombe hilo ikiifunga kwa mikwaju ya penati timu ya Ivory Coast ambayo inatajwa kuwa ni kizazi cha dhahabu cha taifa hilo.

Ivory Coast ya wakati huo ilikuwa ikiongozwa na Didier Drogba, pamoja na nyota wengine kama ndungu Yaya na Kolo Toure, Solomon Kalou, Didier Zokora na Gervinho. Lakini walishindwa kuwafunga Zambia ya akina Stophira Sunzu, Christopher Katongo, Rainford Kalaba, Emmanuel Mayuka na wengineo.

Kundi ambalo linaonekana kufuatia kwa ugumu ni F lenye timu za Benin, Cameroon, Ghana na Guinea Bisau.

Kwa macho ya kawaida, Cameroon na Ghana wanapigiwa upatu kupita kwenye kundi hilo.cameroon

Cameroon ndio mabingwa watetezi wa kombe la Afcon

Cameroon ni mabingwa mara tano wa michuano huku Ghana wameshinda mara nne kombe hilo.

Hata hivyo timu zote za kundi hilozinatokea katika ukanda wa Afrika Magharibi na zinajuana vilivyo katika sampuli zao za uchezaji. Kundi A pia linaonekana jepesi kwa mwenyeji wa michuano hiyo timu ya Taifa ya Misri ambao ni mabingwa wa kihistoria wa michuano hiyo.

Hata hivyo kutakuwa na kipute kigumu si haba baina ya mataifa ya DRC, Zimbabwe na Uganda. Yote kwa yote, hesabu za makundi zitatimia pale michezo hiyo itakapoanza kutimua vumbi Ijumaa. Si ajabu Kenya ama Tanzania zikafuata nyayo za Zambia katika kuangusha timu kubwa kama ilivyotokea mwaka 2012.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents