Promotion

Airtel yazindua SUPA 5, yaleta ofa 5 kabambe kwenye Kuwasiliana, SMS na Intaneti

Airtel Tanzania imezindua ofa 5 kabambe zitakazowafaidisha wateja wake wanaotumia huduma zao za Intaneti (Data) pamoja na huduma ya kawaida ya kuongea na simu pamoja na ile ya kutuma ujumbe mfupi yaani SMS.

Kati ya ofa mpya ziliyozinduliwa ni pamoja na kumwezesha mteja wa Airtel kuongea kwa NUSU Shilingi kwa sekunde siku nzima kwa marafiki Airtel-Airtel, pia wateja wote wataongea kwa ROBO Shilingi kwa sekunde usiku kucha Airtel-Airtel, kujipatia SMS 200 Bure Siku Nzima endapo mteja atatuma SMS10 tu kwa 30Tshs, facebook bure pamoja na kuburudika intaneti ya bure usiku mzima kwa wateja wote watakaojiunga na OFA hii ya Airtel SUPA 5.

Akitoa Mchanganuo kuhusu Airtel SUPA 5 Mkurugenzi Mtengaji wa Airtel Bw Sam Elangalloor alisema “dili hili la ofa 5 za ukweli zinalenga kufaidisha wateja wote wanaotumia huduma za Intaneti na kupiga simu kila wakati. Airtel kipindi hiki tumejipanga kuhakikisha tunawapatia wateja wetu huduma nafuu, bora na zenye ubunifu wa kutosha ili mteja aweze kutimiza malengo yake.

“leo ninaona fahari kuzindua OFA tano kabambe za SUPA 5, Jiunge Upate Raha ya kuwa na mtandao usioficha mambo, Mteja wa Airtel akijiunga na SUPA 5 ataweza kuchagua namba 3 azipendazo au anazowasiliana nazo mara kwa mara na atakuwa anazipigia kwa ½ shilingi tu kwa sekunde siku nzima, pia ataongea kwa ROBO shilingi tu kwa sekunde kwa simu zote atakazopiga Airtel-Airtel usiku mzima. kwa wanaopenda kutuma ujumbe mfupi yaani SMS pia atapata SMS 200 bure mara tu watakapotuma sms 10 kwa Tsh 30, kadhalika huduma ya Internet ni BURE usiku kucha, Vilevile SUPA 5 inakupa uwezo wa kuperuzi mtandao wa jamii yaani Facebook kila wakati BURE” alielezea Bw Elangallor

“Airtel tunaamini kuwa Ofa hizi ni mjumuisho mzuri utakaotoa unafuu kwa wateja wanaperuzi Interneti na facebook mara kwa mara kila wakati, wanaopiga simu pamoja na kutumia ujumbe mfupi kwa kuwasiliana na ndugu na marafiki muda wote” aliongeza Bw, Elangalloor.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Masoko Bw, Cheikh Sarr alisema “ Bado Airtel tutaendelea kuwapa raha wateja na kutoa unafuu kwa wateja wetu kwa kuwa Airtel tunasikiliza wateja na kuitikia kutimiza mahitaji yao kwa haraka, Ninawahakikishia Ofa hizi za Airtel SUPA 5 ni za ukweli ‘hakuna ujanja ujanja’ wala kuficha gharama yoyote kila kitu ni kama unavyosikia.

Ili mteja uweze kuingia na kutumia huduma hii unatakiwa kujiunga kwa kupiga *149*99#. Kisha utapata ujumbe utakaokuhitaji kuchagua muda maalum wa kutumia OFA hii yaani WIKI MOJA au SIKU MOJA, alafu utaweza kujaza namba zako maalum 3 za ndugu, jamaa, au rafiki utakazotaka kuwa unazipigia simu kwa NUSU shilingi siku nzima ndani ya muda wako wa ofa.

Mbali na hilo huduma hii ya SUPA 5 inatoa nafasi kwa mteja yeyote wa malipo ya kabla wa Airtel ambaye amejiunga lakini pia muda wake ukiisha anaweza kujiunga tena kwa mara nyingine, lengo ni kumpa mteja wa Airtel nafasi ya kujiachia kwa unafuu na uhakika zaidi muda wowote na sehemu yoyote nchini Tanzania

Huduma ya Airtel SUPA 5 ni ya kudumu, lengo lake ni kutimiza mahitaji ya wateja wetu nchini bila kujali aina ya simu anayotumia huku tukitoa mawasiliano bora kupitia mtandao wetu ulionea kila mahali nchini Tanzania.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents