Habari

Ajuza wa miaka 103 apona Virusi vya Corona, ajipongeza kwa bia baridi

Ajuza mweye umri wa miaka 103, Jennie Stejna amejipongeza kwa kunywa bia ya baridi aina ya Bud Light, baada ya kupona ugonjwa wa Virusi vya Corona.

Bibi Jennie Stejna aliyejipongeza na bia ya baridi baada ya kupona Corona

Bibi huyo anayepatikana Massachusetts Jijini Boston, alianza kuumwa ugonjwa huo mwanzoni mwa mwezi Mei,  kwa dalili za kukosa ladha pia na kuumwa na homa kisha kupelekwa hospitali.

Kwa mujibu wa TMZ, Daily Mail na vyombo vingine vya habari, Akitoa taarifa hiyo mkwe wa mjukuu wake Adam Gunn amesema, wote walikuwa wanajua tayari wanaelekea kumpoteza bibi yao,  na kuna siku aliwahi kumuuliza kama yupo tayari kwenda mbinguni kisha bibi akamjibu ndiyo.

Easton woman's grandmother, 103, prevails over coronavirus - News ...

Mzee huyo kwa sasa ni mjane na mumewe alifariki mwaka 1992 akiwa na miaka 82, amebahatika kupata watoto wawili, wajukuu watatu, vitukuu wanne na vilembwekezi wanne.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents