Michezo

Akitokea benchi, Firmino awatoa PSG vichwa chini  

Mchezaji wa klabu ya Liverpool, Roberto Firmino ameisaidia timu yake kuchomoza na ushindi wa jumla ya mabao 3-2 mbele ya Paris Saint-Germain michuano ya Champions League hatua ya makundi baada ya kufunga bao lake dakika chache kabla mpira kumalizika.

Katika mchezo huo uliyokuwa na ushindani mkubwa Liverpool ilionyesha uimara wake katika soka msimu huu baada ya kuandika bao la kwanza kupitia kwa Daniel Sturridge dakika 30 tu baada ya mpira huo kuanza kipindi cha kwanza kisha kupata la pili kupitia, James Milner kwa njia ya mkwaju wa penati dakika ya 36.

Ndipo PSG kucharuka na kuanza kulisakama lango la Liver na kupata bao lao la kwanza kupitia kwa Thomas Meunier dakika ya 40 na lapili likiwekwa kimyani na Kylian Mbappe dakika ya 83 hivyo kuufanya mchezo huo kuonekana kama unamalizika kwa sare lakini dakika ya (90+1), Roberto Firmino akitokea benchi akaipatia Liverpool bao la tatu na la ushindi hivyo kuwafanya majogoo hao wa England wakiwa uwanja wa nyumbani Anfield wanafanikiwa kuochomoza na ushinidi wa mabao 3-2.

Kikosi cha Liverpool, Alisson (5), Alexander-Arnold (7), Gomez (6), Van Dijk (7), Robertson (7), Milner (8), Henderson (6), Wijnaldum (8), Mane (6), Salah (5), Sturridge (7)

Wachezaji wa akiba, Shaqiri (5), Firmino (6), Fabinho (5)

Kikosi cha PSG, Areola (5), Silva (6), Kimpembe (5), Meunier (6), Bernat (5), Marquinhos (5), Di Maria (5), Rabiot (6), Mbappe (6), Cavani (5), Neymar (5)

Wachezaji wa akiba, Draxler (5), Choupo-Moting (5)

Mchezaji bora kwenye mchezo huo akiwa ni Georginio Wijnaldum

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents