Burudani ya Michezo Live

Aliyekuwa Rais wa TFF, Michael Wambura aachiwa huru na mahakama, atakiwa kulipa zaidi Sh Milioni 100

Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imemuachia huru aliyekuwa makamu wa Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania(TFF), Michael Wambura kwa masharti ya kutokufanya makosa yoyote kwa kipindi cha miezi 12 nakulipa zaidi ya Shilingi Milioni 100, na laki tisa kwa awamu.

Image
Michael Wambura kwa makubaliano ya kulipa fedha hizo kwa awamu tano hii leo amelipa Shilingi milioni 20,249,531.
Wiki Iliyopita imeripotiwa, Wambura aliiyeleza mahakama hiyo kuwa ameandika kwa Mkurugenzi wa mashitaka nchini (DPP) kwaajili ya kuomba msamaha na kukiri makosa yanayomkabili mahakamani hapo, februari 11 mwaka huu akikabiliwa na kesi ya uhujumu uchumi yenye mashitaka 17 yakiwemo ya kutakatisha zaidi ya Sh. Milioni 100.
Katika mashtaka hayo 17; shtaka moja ni la kughushi, shtaka moja la kutoa na kuwasilisha nyaraka za uongo, mashtaka 13 ya kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu na mashtaka mawili ya kutakatisha fedha haramu katika kesi ya uhujumu uchumi namba 10/2019.

Related Articles

Back to top button
Close
Bongo5

FREE
VIEW