Moto Hauzimwi
TECNO Spark 2

Andre Silva, Griezman, Giroud wang’ara kufuzu kombe la dunia 2018

Timu ya taifa ya Ureno imefanikiwa kutinga katika michuano ya kombe la dunia baada kuchomoza na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Uswizi katika mchezo wa kundi B.

Wachezaji waliyoiwezesha Ureno kutinga katika michuano hiyo mikubwa ni Johan Djourou aliyejifunga na Andre Silva.

Wakati timu ya taifa ya Ufaransa ikifanikiwa kufuzu baada ya kupata ushindio wa mabao 2-1 dhidi ya Belarus na kufanikiwa kuongoza msimamo wa kundi A, na timu ya taifa ya Sweden wakafanikiwa kushika nafasi ya pili katika kundi hilo licha ya kukubali kipigo cha mabao 2-1 dhidi ya Uholanzi.

 

Timu ya taifa ya Uholanzi ilihitaji mihujiza ya ushindi wa mabao 7 mbele ya Sweden ili kufanikiwa kufuzu kwa michuano hiyo jambo ambalo liligonga mwamba na hivyo kuyakosa mashindano hayo huku wapenzi wa mchezo wa soka wakikosa kumshuhudia  Arjen Robben katika michuano hiyo.

Michezo ya kundi H, timu ya taifa ya Ugiriki wamejihakikishia safari ya kombe la dunia baada ya kuchomoza na ushindi wa mabao   4-0 dhidi ya Gibraltar yaliyofungwa na Eden Hazard akifunga mabao mawili, Thorgan na Romelu Lukaku akafunga ukurasa wa mabao.

Mpaka sasa katika mataifa ya Ulaya ambayo yamejihakikishia kushiriki michuano hiyo ni Ufaransa, Ureno, Ujerumani, Serbia, Poland, Uingereza, Uhispania, Ubelgiji na Iceland.

Zimesalia nafasi nne pekee ambazo mataifa manane watazipigania ili kujihakikishia kushiriki ambazo ni Sweden, Uswizi, Ireland Kaskazini, Jamhuri ya Ireland, Denmark, Italia, Ugiriki na Croatia.

Related Articles

Bongo5

FREE
VIEW