Michezo

Arsenal ndiyo inayoingiza mkwanja mrefu zaidi kuliko timu yoyote Ulaya – UEFA

Ripoti ya Shirikisho la soka barani Ulaya (UEFA) iliyotoka hivi karibuni inasema kuwa mashabiki wa klabu ya Arsenal wameonekana kuwa ndiyo wanaoongoza kwa kulipa fedha za viingilio kuliko wapenzi wa timu nyingine zote barani Ulaya na hivyo kuingizia mkwanja mrefu zaidi.

Kufuatia ripoti hiyo  ya UEFA maswali mengi yamezuka kuwa kama Arsenal inaweza kuingiza fedha nyingi kupitia kwa mashabiki wake hali inayopelekea hadi kuongoza timu nyingine zote duniani iweje ishindwe kuwalinda mastaa wake ambao wanaonekana kuondoka kila kukicha huku wengine wakishindwa kuwaongezea mishahara kama kwa Jack Wilshere.

Wilshere akiwa hanafuraha kwakupewa paundi 80,000 kwa wiki na badala yake akihitaji 20,000 

Ripoti iliyotolewa inaonyesha, the Gunners inaingiza kiasi cha paundi 74.09 kwa shabiki mmoja kwa kila mechi. Wakati nafasi ya pili ikishikiliwa na Chelsea ambayo inapata paundi 68.71 katika kila mechi.

Kutokana na thamani ya pesa ambayo Arsenal inaingiza kupitia kwa mashabiki wake inasikitisha kuona timu hiyo inashindwa kufanya vizuri ndani ya Uwanja huku klabu ikiwa bado inauza wachezaji wake bora na ambao wapo katika kiwango kwa sasa.

 

Alexis Sanchez akikaribia kutua Manchester United wakati bado timu yake ya Arsenal ikiwa katika vuguvugu la kuondokewa na baadhi ya wachezaji wake muhimu.

Theo Walcott akitarajia kujiunga na Everton wiki hii kwa dili la paundi milioni 25 hii ni baada ya kukamilisha vipimo vya afya

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents