Michezo

Asante Kwasi atema cheche Mapinduzi Cup

Beki mpya wa klabu ya Simba Mghana, Asante Kwasi hapo jana amefanikiwa kufunga bao lake la kwanza katika mchezo wake wa kwanza akiwa anaitumikia timu hiyo toka asajiliwe katika dirisha hili la mwezi wa kwanza akitokea Lipuli FC.

Kwasi ambaye usajili wake umetikisa vichwa vya habari hapa nchini amewahi kuitumikia klabu ya Mbabane Swallows ya Swaziland kabla ya kujiunga na Lipuli FC.

Mghana huyo anayecheza nafasi ya ulinzi ameshinda bao hilo katika mchezo wa Kombe la Mapinduzi dhidi ya timu ya Jamhuri huko Visiwani Zanzibar na kufanya Simba SC kuchomoza na na ushindi wa mabao 3-1.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents