Burudani

AT afungukia kauli ya Dkt. Mwakyembe

AT ameonyesha kupingana na kauli ya Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe kusema wasanii waachane na tabia ya kuimba nyimbo za kisiasa kwa kuwatolea mifano wasanii wa Nigeria akiwemo P Square, Don Jazzy, Tiwa Savage na Davido.

Japo muimbaji huyo hajaweka wazi kuhusu hilo, amepost kipande cha video kwenye mtandao wa Instagram huku akisema, “Watanzania, tatizo la mitandao sio tatizo kubwa kama tatizo la kujua kwingi. Mpeni salamu mjomba wakati, mwambieni sanaa haijakuta siasa ila siasa ndio imeikuta sanaa.”

“Kuzungumzia maisha ya wasanii wa Nigeria ambao serikali yao inategemea sanaa na mafuta, serikali yetu inategemea madini na utalii. Pointi yako haikuwa na mashiko hata kidogo, mpaka umefikia kuwajua kina Davido na Don Jazzy kwa sababu ya sanaa ila wao hawakujui wewe kwa sababu ya siasa,” ameongeza kwenye video hiyo.

Msanii huyo pia amesisitiza kwa kuandika, “Msanii mmoja ambae ni mwanasaikolojia pia ni mwana harakati kutoka visiwani zanzibar anaejulikana kwa jina la Ali Ramadhani alisema maneno haya (Sio Sababu wewe ni waziri wa michezo basi ukaona ufanye mchezo ktk kitu kisichokua cha mchezo maana michezo huleta mambo sio ya mchezo mchezo) Elimu ni mbwembwe Upeo ndio kila kitu #Mjinganiyuleanaejifanyaanajuakilakitu..! SIASA ZIMEUKUTA MUZIKI.”

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents