Michezo

Atletico Madrid yatwaa ubingwa wa UEFA Super Cup, Costa man of the match

Klabu ya Atletico Madrid imefanikiwa kutwaa ubingwa wa UEFA Super Cup baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 4-2 dhidi ya hasimu wake Real Madrid.

Mchezo huo uliyopigwa kwenye dimba la Le Coq Arena umeshuhudiwa ukienda sare ya magoli 2-2 ndani ya dakika 90 hivyo kulazimika kupigwa dakika za nyongeza ambazo Atletico walizitumia vema na kuibuka na ushindi huo wa mabao 4-2.

Diego Costa alikuwa mwiba mkali kwa upande wa Madrid kwa kuisaidia timu yake ya Atletico kupata bao la mapema kabla hajafunga la pili dakika ya 79 wakati Madrid ikipata mabao yake kupitia kwa Benzema dakika ya 27 na Sergio Ramos dakika 63 matokeo yaliyofanya mechi hiyo kwenda sare ya 2-2 katika dakika hizo 90.

Katika dakika za nyongeza Atletico walikuja kivingine na hivyo kuizidi mbinu za kiufundi Madrid na kupata magoli mawili kupitia kwa Saul Niguez dakika ya 98 na Koke akifunga kunako dakika ya 104 hivyo kuufanya mchezo huo uliyokuwa wakuvutia na ushindani mkubwa kumalizika kwa matokeo ya mabao 4-2.

Vikosi vya timu zote mbili Real Madrid: Navas (5), Carvajal (5), Ramos (6), Varane (5), Marcelo (6), Kroos, Casemiro (5), Asensio (6), Isco (5), Benzema (6), Bale (6)

Wachezaji waakiba : Modric (6), Ceballos (5), Lucas Vazquez (5), Mayoral (5)

Atletico Madrid: Oblak (6), Juanfran (6), Savic (7), Godin (7), Hernandez (7), Saul (7), Koke (7), Rodrigo (7), Lemar (7), Costa (8), Griezmann (6)

Wachezaji waakiba : Correa (7), Vitolo (7), Thomas Partey (7), Gimenez (NA)

Aliyeibuka mchezaji bora wa mechi hiyo ni Diego Costa.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents