Michezo

Aubameyang kumpokonya mtu namba Barcelona, Zlatan Ibrahimovic kumfuata Ronaldo

Mshambuliaji mwenye maneno mengi kunako klabu ya LA Galaxy, Zlatan Ibrahimovic anajiandaa kurudi katika ligi ya Italia Serie A ambayo pia yupo mchezaji nyota kwa sasa Cristiano Ronaldo.

Image result for zlatan ibrahimovic

Kwa mujibu wa (ESPN, via Calciomercato) anatarajiwa kutua katika klabu ya AC Milan, ambayo inaonekana hapo vizuri kwa sasa ikishika nafasi ya 11 kwenye msimamo wa Serie A .

Mshambuliaji Erling Braut Haaland 19, anaweza kujiunga na klabu RB Leipzig akitokea Red Bull Salzburg msimu ujao pamoja na kutolewa macho na Manchester United, Liverpool na Arsenal. (Sky Sports)

Barcelona imesema ina nia ya kumsajili mshambuliaji wa Gabon Pierre-Emerick Aubameyang, 30, kutoka Aresnal itakapofika mwezi Januari.(El Chiringuito via Mirror)

Manchester United, Tottenham na Wolves wanawania saini ya mshambuliaji James Rodriguez,28, wa Real Madrid mwezi Januari.(El Desmarque – in Spanish)

Crystal Palace wanafuatilia maendeleo ya mshambualiaji Wout Weghorst,27 ambaye amefunga magoli manane katika michezo 15 akiichezea Wolfsburg.(Calciomercato – in Italian)Erling Braut HaalandMshambuliaji Erling Braut Haaland

Arsenal watapambana na West Ham kumsajili mchezaji wa nafasi ya ulinzi Martin Hinteregger, 27, wa Eintracht Frankfurt. (Sun)

Bournemouth na Wolves wana nia ya kumpata mshambuliaji wa Huddersfield Karlan Grant mwezi Januari.(Sun)

Bayern Munich haitamteua Arsene Wenger kuwa kocha wake ingawa kocha huyo wa zamani wa Arsenal ameeleza nia yake ya kuwa kocha wa Bayern Munich alipokuwa akizungumza kwa njia ya simu na mwenyekiti wa klabu. Karl-Heinz Rummenigge. (Sky Sports)

Mkurugenzi wa michezo wa klabu ya Paris St-Germain Leonardo amesema kauli ya kocha wa Real Madrid, Zinedine Zidane kuwa mshambuliaji wa timu ya taifa ya Ufaransa Kylian Mbappe, 20, kuwa ana ndoto ya kuchezea mabingwa hao wa La Liga ni ya ”kuudhi”.Pierre-Emerick AubameyangMshambuliaji wa Gabon Pierre-Emerick Aubameyang

Mchezaji wa nafasi ya ulizi ya Southampton Cedric Soarea amesema ataondoka kwenye klabu hiyo mwishoni mwa msimu. (Telegraph)

Mchezaji wa zamani wa Manchester United na Skauti wa Juventus amesema kuwa kiungo Paul Pogba,26, ataenda kwenye timu ya Italia.(Tuttosport, via Goal)

Mchezaji wa nafasi ya ulinzi wa timu ya Arsenal Kieran Tierney, 22, amesema ni juu ya wachezaji wenyewe uwanjani kutatua matatizo ya klabu yanayoendelea. (Telegraph)

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents