Audio: Masau Bwire amtaka kocha wa Barcelona kuja Tanzania kujifunza kwa Ruvu Shooting

Msemaji machachari wa klabu ya Ruvu Shooting, Masau Bwire amesema kuwa Azam FC  wanapaswa kumshukuru Mungu kwa kushusha mvua ya enzi za Nuhu hapo juzi kwenye uwanja wa Mabatini, Pwani lasivyo wangewapapasa zaidi ya usindi wa mabao 2 – 0 waliyopata hapo jana kwenye mchezo wao wa ligi kuu soka Tanzania Bara huku akisema kuwa laiti kocha wa Barcelona angetazama mechi hiyo angekuja Tanzania kujifunza mawili matatu kutoka kwao.

 

Msemaji huyo wa Ruvu Shooting, Masau Bwire ameyasema hayo hapo jana kupitia kipindi cha michezo cha Magic Fm wakati akizungumzia namna alivyopokea ushindi wao dhidi ya Azam FC.

Nilishazungumza kwamba jana (juzi) kama mechi ingeweza kuchezwa tulikuwa tumechungulia na tayari ingekuwa zipigike nne lakini Mungu akaepusha hilo akaona Azam FC hawa kwanamna walivyo wakifungwahizo ni hatari akashusha mvua za enzi za Nuhu mechi ikashindikana kuchezwa.

Sasa leo kilichofanyika nilisema tangu jana hana namna lazima apapaswe na kweli idadi imepungua kidogo lakini ikatosha Azam FC leo mbele ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani aliyeongozana na mkuu wa wilaya ya kisarawe hadhjarani mbele ya umati wawatu waliyokuja kushuhudia mpambano huu akapapaswa.

Tumemzidi kila hali, kila idara vijana wamecheza mpira wa kiwango na ubora wa hali ya juu sana mpaka ikafikia wakati watu wakaanza kujadili kocha wa Barcelona angekuwa anautazama huu mpira pengine angetaka kuja Tanzania kutaka kujua nani huyu anaewafundisha Ruvu Shooting mambo makubwa haya na pengine ajifunze mambo mawili matatu kutoka Ruvu Shooting.

EXCLUSIVE: Mchezo wa Ruvu Shooting Vs Azam FC waahirishwa kufuatia maji kujaa dimba la Mabatini, Pwani (Video)

Video: Masau Bwire atoa siri kutembea na rundo la simu

Baada ya ushindio huo mnono wa Ruvu Shootingi dhidi ya Azam FC umeifanya timu hiyo kutoka nafasi ya 10 hadi ya saba kwenye msimamo wa ligi kuu soka Tanzania na hivyo kujaribu kuepukana na kitendo cha kushuka daraja.

Related Articles

Bongo5

FREE
VIEW