Michezo

Azam FC yatoa msaada kwa watoto yatima kabla kuivaa Mbao

Ikiwa imesalia siku moja kabla ya kikosi cha Azam FC hakijakabiliana na Mbao, Mabingwa hao wa Afrika Mashariki na Kati hii leo wametembelea kituo cha watoto yatima cha Sekondari ya Ilemela Islamic Seminary, kilichopo Ilemela mkoani Mwanza.

Mabingwa hao wanatarajia kumeanyana na Mbao kesho Jumamosi katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara (VPL) utakaofanyika Uwanja wa CCM Kirumba.

Huo ni mwendelezo wa klabu hiyo katika kujenga mahusiano mazuri na jamii kwa kujali watu wenye mahitaji mbalimbali, ambapo mwishoni mwa mwaka jana ilitoa msaada kwa baadhi ya wakazi wa mkoa wa Kagera walioathirika na tetemeko la ardhi ilifanya hivyo siku kadhaa kabla ya kukabiliana na Kagera Sugar na kufanikiwa kushinda kwa mabao 3-2.

Zoezi hilo limehudhuriwa na msafara wote wa Azam FC uliowasili mkoani Mwanza, ambapo wamepokelewa kwa heshima kubwa na viongozi wa seminari hiyo wakiongozwa na Meneja na Makamu Mwenyekiti, Sherally Hussein Sherally.

Azam FC haijaiacha mikono mitupu Seminari hiyo inayotoa elimu ya awali, msingi na sekondari kwa ngazi zote mbili, kwani imetoa msaada wa katoni 10 za Maji safi ya Uhai Drinking Water, Katoni mbili za Juice za boksi za Azam na mbili nyingine za kopo pamoja na pakiti mbili za pipi.

Uongozi wa seminari umeipongeza na kuishukuru timu hiyo na Kampuni kwa ujumla ya Azam kwa moyo wa huruma waliouonyesha na kuitakia mafanikio mema kwenye mechi wanazocheza.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents