Michezo

Azam wampeleka kwa mkopo, Mbaraka Yusuph timu ya daraja la kwanza Namungo FC

Klabu Bingwa ya Afrika Mashariki na Kati, Azam FC imeamua kumpeleka kwa mkopo mshambuliaji wake, Mbaraka Yusuph katik timu ya Namungo inayoshiriki ligi daraja la kwanza.

Nyota huyo aliyewahi kuwa mfungaji bora ‘top score’ wa ligi kuu kwa miezi tofauti na hata kufanikiwa kutwaa tuzo ya mchezaji bora chipukizi msimu wa mwaka 2017/18 amejikuta akisumbuliwa na majeraha hali iliyopelekea kushuka kwa uwezo wake.

Taarifa za ndani ya klabu ya Azam zinasema kuwa kupelekwa Mbaraka Yusuph katika timu hiyo ya daraja la kwanza ya Namungo ni maamuzi ya mwalimu na uongozi.

Namungo FC ni timu ya Wilaya ya Ruangwa mkoani Lindi iliyoanza mwaka 2009 ikiwa kama sehemu ya mazoezi kwa wachimbaji madini waliyokuwa wakitoka kazini.

Mbaraka Yusuph mewahi kugonga vichwa vya habari mbalimbali hasa juu ya uwezo wake wa kucheza mpira na sakata lake la usajili kwabaadhi ya klabu kongwe nchini ikiwemo Simba na Yanga kabla kujiunga na Azam FC.

Azam FC ilimsajili nyota huyo mwenye malengo ya kucheza soka la kulipwa katika klabu za Madrid na Barcelona za nchini Hispania akitokea Mtibwa Sugar

Katika moja ya mahojiano yake na vyombo vya habari Mbaraka amewahi kuweka wazi ndoto hizo za kuzichezea miamba hiyo ya soka ya Hispania hukua akisema kuwa nia yake ni kufuata nyayo za mshambuliaji wa Taifa Stars, Mbwana Samatta ambaye anakipa Ubelgiji kwenye klabu ya KRC Genk.

Mbaraka Yusuph aliyeibukia kikosi B cha Simba na kwenda Kagera Sugar, alimaliza nafasi ya pili ya ufungaji bora msimj wa mwaka 2017/18 akiwa na jumla ya mabao 13, nyuma ya Saimo Msuva na Abdulrahman Mussa.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents