Moto Hauzimwi
TECNO Spark 2

Baada ya kukatisha tamasha lake 2016 , Kanye West adai alipwe fidia

Kampuni ya rapper Kanye West imeitaka kampuni ya Lloyd iliyopo nchini Uingereza, imlipe rapper huyo kiasi cha dola milion 9.8 kwa kukatisha tamasha la Saint Pablo mwaka jana.

Kwa muijibu wa taarifa zilizotolewa na Very Good Touring (VGT), zinaeleza kuwa mnamo mwaka 2016 Novemba, kampuni ya Kanye iliwaliandikia ombi kampuni ya Lloyd kuvunja mastamasha yaliyosali ya rapper huyo baada ya kupatwa na maradhi yaliyopelekea alazwe hospitali kwa muda wa siku nane.

Hata hivyo kampuni hiyo haikufanya kama walivyoambiwa na kampuni ya Kanye na wakadai kuwa rapper huyo amejichanganya mwenyewe kwani alikuwa ametumia madawa kulevya aina ya bangi ili asiendelee na tamasha, kufuatia hali hiyo VGT wamedai malalamilo ya Lloyd sio ya kweli na hayana ushaidi wa kutosha ila wanachotakiwa kufanya kwa sasa ni kumlipa rapper huyo.

Na Laila Sued

Related Articles

Bongo5

FREE
VIEW