Burudani

Baada ya Marekani na UK, Rayvanny kukisanua Tanzania

Msanii wa muziki Bongo kutoka WCB, Rayvanny amefunguka sababu ya kufanya show nyingi zaidi nje kuliko Bongo.

Muimbaji huyo amesema kinachopelekea hilo ni kutokana waandaji wengi wanaojitokeza ni kutoka nje ya nchi ila kuna mpango wa kufanya tour Tanzania.

“Namshukuru Mungu nilikuwa na tour UK, Marekani lakini pia nina mpango mwaka huu kuwa na tour nyingine, kuna watu ambao tumeongea nao kuna mipango ya kufanya Tanzania nzima,” Rayvanny ameiambia Bongo5.

“Show nyingi tunafanya sana nje sijajua ni sababu gani lakini inatokea hivyo lakini mwaka huu nitafanya tour Tanzania baada ya kumaliza Marekani,” ameongeza.

Rayvanny kwa sasa anafanya vizuri na ngoma ‘Pochi Nene’ ambayo amemshirikisha producer S2kizzy.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents