Michezo

Baada ya mchezo na Yanga, Simba wapeleka malalamiko TFF, Wizarani (Video)

Klabu ya soka ya Simba imeandika barua kwa Shirikisho la soka Tanzania (TFF), Bodi ya Ligi na Wizara ya Michezo kueleza malalamiko yao ya kutoridhishwa na maamuzi ya waamuzi katika michezo yake ya Ligi Kuu soka Tanzania bara msimu wa 2017/18.

Hayo yamesemwa na Mkuu wa Kitengo cha Habari na Mawasiliano wa klabu ya Simba, Haji Manara leo mchana alipozungumza na waandishi wa habari.

Manara amesema nakala za barua hiyo wamezipeleka TFF, Bodi ya ligi TPLB pamoja na kwa Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe kuhusiana na uamuzi wa kutoridhishwa kwa baadhi ya waamuzi katika michezo mbalimbali ambapo kikosi cha Simba kimekuwa kikishuka dimbani.

“Tumeandikia barua kwa Shirikisho tukieleza dhuluma tunayofanyiwa na waamuzi pia nakala nyingine tumetuma kwa waziri mwenye dhamana ya michezo kwasababu haturidhishwi na maamuzi kwenye mechi zetu”, amesema Manara ambaye ni mkuu wa kitengo cha habari wa Simba SC.

Baadhi ya michezo ambayo klabu ya Simba imeonyesha kuchukizwa na maamuzi ni kunyimwa kwa Penati dhidi ya Yanga SC siku ya Jumamosi iliyopita wakati beki Kelvin Yondani alionekana kuushika mpira.

Michezo mingine ambayo Simba SC imelalamikia maamuzi yaliyofanywa ni pamoja na Stand United na Mbao FC.

Katika upande mwingine Manara ameeleza ratiba ya kikosi cha Simba SC kuwa kinatarajia kwenda mkoani Mbeya Novemba 3 kwa ajili ya mchezo wake dhidi ya Mbeya City siku ya Jumapili wakati ikiwa huko itacheza mchezo mmoja wa kirafiki kabla ya kuvaana na vijana hao wa Jiji la Mbeya.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents