DStv Inogilee!

Baada ya ushindi huu wa Simba, Mbabane Swallows watatakiwa kufunga idadi hii ya mabao kumtoa Mnyama

Mabingwa watetezi wa ligi kuu soka Tanzania Bara Simba SC imefanikiwa kuibuka na ushindi mnono wa jumla ya mabao 4 – 1 dhidi ya Mbabane Swallows katika michuano ya klabu bingwa Afrika.

Katika mchezo huo John Bocco amefanikiwa kufunga jumla ya mabao mawili katika kipindi cha kwanza dakika ya nane na 32,kisha nyota wao Meddie Kagere akifanikiwa kufunga la tatu dakika ya 84 na Clatous Chama akihitimisha karamu ya magoli kwa kufunga dakika ya 90+2 huku lakufutia machozi la Mbabane likitiwa kimyani na Nzambe dakika ya 24.

Mchezo huo uliyokuwa wa kipekee kwa Simba umeshuhudia muwekezaji wao Mohammed Dewji akiwa miongoni mwa watu waliyokwenda kuwashuhudia uwanjani na kuwapa nguvu ikiwa ni mara yake ya kwanza kufanya hivyo toka apatwe na tatizo la kutekwa kisha kupatikana mwezi Oktoba mwaka huu.

Kutokana na matokeo hayo Mbabane Swallows watalazimika kuibuka na ushindi wa jumla ya mabao 3 – 0 kwenye mchezo wa marudiano dhidi ya Simba ili kujihakikishia wanasonga mbele na kumtoa Mnyama.

Related Articles

Back to top button
Bongo5

FREE
VIEW