Habari

Barack Obama na Michelle watuma salamu za pongezi kwa Prince William na Kate

Aliyekua rais wa Marekani, Barack Obama na mkewe Michelle Obama wametuma salamu za pongezi kwa Prince William (Duke of Cambridge) na mkewe Kate Middleton (Duke of Duchess) kwa kupata mtoto wao wa tatu.

Taarifa hiyo imeandikwa na Michelle kupitia mtandao wake wa Twitter huku akisisitiza kuwa watadai kuwa watahudhuria kwenye sherehe ya mtoto huyo itakayofanyika kwenye jumba la Malkia (Kensington Palace).

“Barack and I are thrilled to congratulate The Duke and Duchess of Cambridge on their newest arrival! We hope to meet him soon for a Kensington Palace pajama party. I’ll wear my robe!,” ameandika Michelle.

Kate Middleton alijifungua mtoto huyo wa kiume Jumatatu hii kwenye Hospital ya St. Mary’s.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents