DStv Inogilee!

Barakah The Prince awakatisha tamaa mashabiki kuhusu kolabo zake za Sauti Sol na Cassper Nyovest (+Audio)

Ulikuwa unahamu ya kuzisikia kolabo za Barakah The Prince alizofanya na Sauti Sol na Cassper Nyovest? Hilo unatakiwa kusahau tena.

Barakaha aliwahi kusema kuwa tayari ameshafanya kolabo kibao na mastaa wakubwa Afrika na kutuhakikishia kuwa ngoma hizo zitapatikana kwenye albamu yake, lakini kwa sasa ameonyesha ni vigumu kuzisikia tena ngoma hizo.

Akiongea na mtangazaji wa Jembe FM, JJ amesema, “Hizo zilikua ni project ambazo zilikuwa under Rockstar kipindi ambacho nilikuwa yao. Ni nyimbo ambazo wanazishikilia wao, walinilipia kila kitu kutoka hapa na kwenda Kenya na kila kitu Production, Producer na kila kitu. Sauti Sol makubaliano yao mikataba. Tulisaini mkataba kabla hatujarekodi, kwa hiyo ilikuwa ni product ya kwao kina Seven.”

“Nimejaribu kuongea nao kupatiwa hizo nyimbo, kulikuwa na ngoma ya Cassper kuna Sauti Sol, wamezing’ang’ania kwa sababu zao wao,” ameongeza.

Related Articles

Back to top button
Bongo5

FREE
VIEW