Tupo Nawe

BBA Updates: Rapper Ice Prince wa Nigeria awasuprise washiriki kwa kuwatembelea mjengoni leo

Washiriki wa ‘The Chase’ mchana huu wamepata ugeni wa kushtukiza wa rapper Ice Prince kutoka Nigeria ambaye ametia timu katika jumba la Big Brother kama balozi wa One Campaign na kupiga story na housemates wanaoendelea kuzi chase $300,000 za Biggie.

Ice prince

Washiriki wa Ruby walishindwa kuzuia furaha zao mara baada ya kumuona star huyo aliyeingia mjengoni kwa style ya aina yake bila taarifa.

Ice Prince ambaye ametembelea nyumba ya Big brother kama balozi wa One Campaign kwa kushirikiana na African Union, ametumia uwepo wake katika nyumba hiyo kuchat na washiriki pamoja na kuwahamasisha kujihusisha na huduma za kijamii hata wakiwa nje ya Big Brother watakapokuwa wamerejea katika nchi zao.

Ice Prince ambaye jina lake halisi ni Panshak Zamani, ameendelea kuwaeleza washiriki kuwa sasa wamekuwa mastaa nje ya mjengo hivyo wajitahidi kutumia ukubwa wa majina yao kwa faida ya jamii.

“Whether you win the money or not you guys should get involved, hopefully by 2030 extreme poverty should be eradicated. Your voices and your images will do that in a lot of ways”. Alisema Ice Prince

Related Articles

Back to top button
Close
Bongo5

FREE
VIEW