Burudani

BBA Updates: Tanzania yaiaga rasmi ‘The Chase’ baada ya safari ya Feza kufikia ukingoni

Hatimaye safari ya Tanzania katika Big Brother ‘The Chase’ imefikia tamati jana (August 11) baada ya mshiriki pekee aliyekuwa amesalia Feza Kessy kutolewa.
feza out

Feza ambaye amefanikiwa kudumu kwenye mchezo kwa siku 77 amekuwa mshiriki wa 20 kuliaga shindano hilo huku Cleo na Dillish waliokuwa dangerzone wakibaki salama.

Feza aliyekuwa ameshikilia bendera ya Tanzania wakati wa eviction hakuonekana kushtuka sana baada ya mtangazaji wa eviction show IK kumtaja kuwa ndiye anayefungasha mizigo, huenda kwasababu tayari alikuwa ameshakata tamaa ya kubaki toka wiki iliyopita.

Matumaini ya Feza yalionekana kufifia kuanzia eviction ya wiki iliyopita ambayo hakuamini kuona amebaki huku kipenzi chake Oneal akitolewa, lakini katika dairy session ya jana jioni masaa machache kabla ya eviction pia alisikika akimwambia biggie “I feel like it is over for me,” baada ya Biggie kumuuliza alimaanisha nini aliposema “I have lost hope but not in a bad way I think it is a defence mechanism”.

Nguvu ya ushindi kwa Feza ilianza kupungua siku kadhaa baada ya kuzama kwenye mapenzi na Oneal kiasi cha kuwafanya washiriki wenzao kuwaona wanajitenga muda mwingi na kujisahahu kuwa wapo mchezoni.

Moja ya maswali ambayo IK alimuuliza Feza baada ya kutoka ni kama bado anampenda Oneal, na jibu lilikuwa “Yes I do”, je unadhani hii inamaanisha kuna kitakachoendelea sasa baada ya ONEZA wote wawili kurudi katika maisha yao ya kawaida?

Baada ya Feza kuondolewa katika The Chase sasa Tanzania inaungana na Kenya na Uganda kubaki kuwa watazamaji baada ya washiriki wote wa Afrika mashariki kutolewa.

Nigeria ndio nchi pekee ambayo mpaka sasa washiriki wake wote wawli Melvin na Beverly bado wako mchezoni wakiwa ni miongoni mwa washiriki 7 waliosalia huku zikiwa zimesalia siku 13 kufika fainali. Unahisi nani ataondoka na $300,000 za Big Brother mwaka huu?

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents