Soka saa 24!

Beka Ajipanga kushoot Video

Beka

Msanii wa Muziki wa Kizazi kipya (Bongo Flava) Bakari Hassan au Beka, ambaye kwa sasa anatamba na Kibao chake kiitwacho Natumaini Remix, anatarajia kuanza kurekodi video ya wimbo huo na kudai kuwa itakuwa moto wa kuotea mbali.

Akizungumza na Bongo5, Beka alisema muda wote tangu kuachiwa kwa Singo hiyo alikuwa akitazama ni jinsi gani itaHIT katika vyombo vya Redio na Television na kwamba hadi sasa ameamini kuwa kweli imekuibalika.

Alisema umefika wakati wa wapenzi wa Burudani kufumbua macho yao kuisubiri ‘Ngoma’ hiyo na kwamba Darubini zake zinaonyesha itabamba miongoni mwa Video bora nchini.

Alisema pamoja na hilo ana imani kuwa  wimbo huo katika siku zijazo utachaguliwa kuwa moja ya wimbo bora wa R n’B  hapa nchini kutokana na vionjo mbalimbali vilivyomo ndani ya tungo hiyo aliyodai kuwa ni ya kisasa.

Aidha Beka amewaomba watu wengi na zaidi Wadada zetu kujitokeza kwa wingi katika uchukuaji wa vipande vya video hiyo vinayotarajiwa kupigwa maeneo mbalimbali ya Jiji la Dar es salaam.

Sikiliza ngoma hiyo hapa

Related Articles

Back to top button
Bongo5

FREE
VIEW