Habari

Waathirikia wazidi kupata Misaada

Wafanyakazi wa Shirika la msalaba mwekundu wakipanda misaada ya nguo iliyotolewa na watu mbalimbali

Shirika La Msalaba Mwekundu imendelea kupokea misaada mbalimbali kwa ajili ya waathirika wa milipuko ya Mabomu iliyotokea Februari 16 Mwaka huu katika Kambi ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) kikosi cha 511 eneo la Gongolamboto.

Misaada iliyopokelewa ni pamoja na fedha taslimu ,nguo, Sahani na Vikombe, Mataulo ya Kike (Peds), Sabuni za kuogea na kufulia, Mahema, Vyakula na vingine vingi.

Katibu Mkuu Msaidizi wa Shirika la Msalaba Mwekundu Peter Mlebusi, kushoto, akipokea msaada wa kiasi cha Sh.milioni 1.5
Katibu Mkuu Msaidizi wa Shirika la Msalaba Mwekundu Peter Mlebusi, kushoto, akipokea msaada wa kiasi cha Sh. milioni 1.5

Akipokea misaada hiyo Katibu Mkuu  Msaidizi wa  Shirika hilo, Bw. Peter Mlebusi,alisema bado misaada zaidi inahitajika kwa waathirika hao na pia kwa kiasi fulani wanaendelea kutatua matatizo yanayowakabili.

Alisema hali ilivyo sasa bado kuna idadi kubwa ya waathirika hao inayohitaji misaada mbalimbali hivyo watu wenye uwezo na hata wasio nao wajitokeze kutoa misaada hiyo.

Hapa Mkurugezi akipokea misaada ya vyandarua
Hapa Mkurugezi akipokea misaada ya vyandarua

Aidha alisema kutokana na milipuko hiyo, Familia zaidi ya 378 ziliathirika na nyumba zipatazo 22 zilivunjwa kabisa na milipuko na kwamba wanawake wapatao 204 waliathirika pamoja na watoto 111.

Aklisema pia watoto 847 walipotea ama kupotezana na wazazi wao ambapo hadi hivi sasa tayari watoto 828 wamepatikana na kukabidhiwa kwa wazazi  huku wengine 18 wakiendelea kulelea katika vituo mbalimbali wakisubiri kukuitanishwa na wazazi wao.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents