Burudani

Ben Pol kuzindua ramsi video ya ‘Sophia’ Jumapili hii New Maisha Club

Video ya muimbaji wa R&B Benard “Ben Pol” Paul imekamilika na tayari amekabidhiwa mkononi na muongozaji wa video hiyo Khalfani.

Ben pol

Ben Pol amesema kuwa anatarajia kuizindua rasmi video hiyo Jumapili hii April 19 kwenye ukumbi wa New Maisha Club.

“Muda ambao tutakuwa tunaitambulisha pale Maisha ndo muda huo huo watu wanaweza kuipata Youtube” ameiambia Bongo5.

Ameongeza kuwa uzoefu mkubwa alioisha upata kutokana na video alizoishafanya ulimfungua mawazo na kufanikiwa kupata wazo lililotumika kufanya video ya ‘Sophia’ pasipo kutumia gharama kubwa.

“Mimi na timu tuliwaza kwamba video nzuri sio lazima iwe ya hela nyingi, bali iwe na wazo zuri pamoja na vifaa vya kuliwezesha lile wazo liweze kutimia.”

Video ya Sophia ilifanyika mkoani Dodoma.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents