Michezo

Benni McCarthy avamiwa na majambazi Johannesburg na kuporwa

Mshambuliaji wa zamani wa Afrika Kusini na vilabu vya Porto na Blackburn, Benni McCarthy mwenye rekodi ya kufunga magoli amevamiwa na watu watatu wenye silaha na kuporwa.

benni1

McCarthy, kwa sasa anaishi jijini Johannesburg akiwa kama mchambuzi wa soka kwenye kituo cha televisheni.

Rafiki wa karibu wa McCarthy, Percy Adams, ambaye alikuwa naye wakati huo, aliiambia PowerFM: Mtu mmoja alimfuata Benni na kumuwekea bunduki sikioni. Alimwambia ampe saa na hereni.”

“Benni aliziba mkono wake mmoja kuficha pete yake ya ndoa kwa sababu ni kitu cha thamani kwake. Mtu mmoja aliiona na kusema; “Nipe pete na Benni aliamua kumpa.”

Polisi wanafanya uchunguzi wa tukio hilo ambalo limekuja miezi sita baada ya mlinda mlango wa Afrika Kusini Senzo Meyiwa kupigwa risasi akiwa mjini Soweto.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents