Burudani

Tunampenda TID, tumsaidie kumtoa kwenye matumizi ya unga – Q-Chief

Q-Chief amedai kuwa ni muhimu jitihada zikafanyika na wadau mbalimbali ili kumuokoa TID kutoka kwenye dimbwi la matumizi ya madawa ya kulevya.

11049372_823677941038866_1799473443_n

TID amekuwa akihusishwa kutumia dawa kwa kipindi kirefu lakini ameendelea kukanusha.

Akiongea kwenye kipindi cha Harakati cha Clouds TV kinachoendeshwa na Kalapina, Chief alisema TID ni msanii mwenye uwezo mkubwa hivyo ni muhimu kwa watu kumshawishi kuachana na matumizi ya dawa hizo kama yeye alivyofanikiwa kuacha.

TID ni Q-Chief waliwahi kuwa maswahiba wa muda mrefu na walikuwa pamoja kwenye Top Band japo walikuja kukosana. Hadi sasa hawaelewani na kauli hii ya Q-Chief inaweza ikawa ni mwiba kwa Top in Dar!

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents