Burudani

Big Brother Africa: Angola yaiaga ‘The Chase’ baada ya washiriki wake wote wawili kutolewa

Jana Jumapili (June 16) ilifanyika Eviction show katika reality show ya Big Brother Africa ‘The Chase’ inayoendelea kule Afrika Kusini, na wiki hii ilikuwa ni zamu ya Angola kupunga mkono wa kwaheri baada ya washiriki wake wote wawili kushindwa kupata kura za kutosha kuwafanya waendelee kuwakilisha nchi yao katika shindano hilo.

B & N

Biguesas na Neyll wa Angola ndio waliofungasha mizigo yao usiku wa jana baada ya safari yao ya kuifukuzia $300,000 kufikia mwisho na kufanya nchi ya Angola iungane na Uganda kubaki kuwa watazamaji baada ya washiriki wao wote kuwa nje ya mchezo.

Biguesas ndiye aliyekuwa wa kwanza kutajwa na mtangazaji wa Eviction show IK, akifuatiwa na mwenzie Neyll. Inavyoonekana Neyll ndiye aliyewagusa zaidi washiriki wengine kutokana na jinsi ambavyo washiriki wa nyumba zote mbili Diamond na Ruby walivyopata mshtuko baada ya IK kutaja jina lake kuwa ndie mshiriki wa pili anaefungasha mizigo yake na kurudi Angola.

Walikuja pamoja na wapiga kura wameamua warudi wote nchini kwao, tusubiri kuona ni kina nani watakaoingia ‘danger zone’ wiki hii ikiwa ni wiki ya nne toka msimu wa 8 wa shindano hilo uanze.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents