Burudani

Big Brother Africa: Feza Kessy aponea chupuchupu, Uganda imeaga shindano, South Africa na Kenya matatani!

Jumapili ya (June 9) imefanyika evication show ya pili katika Big Brother ‘The Chase’ ambayo kama zisingekuwa kura za nchi tatu kumuokoa mshiriki wa Tanzania Feza Kessy, basi huenda hivi sasa angekuwa anajiandaa kufanyiwa shopping ya kifuta machozi na Big Brother huku akijiandaa na safari ya kurudi Tanzania, lakini yuko salama.

LK4 & Koketso

Ndoto za kushinda kitita cha $300,000 zilifikia ukingoni kwa couple ya LK4 mshiriki wa Uganda aliyekuwa amesalia pamoja na Koketso wa Afrika Kusini ambaye hata hakujua kama alikuwa nominated kutoka.

Ikiwa ni wiki ya tatu ya Big Brother ‘The Chase’ Uganda imeshauaga rasmi mchezo baada ya washiriki wake wote wawili kutoka na kuziacha nchi za Kenya na Africa kusini zikipumulia mashine kwa kubaki na mshiriki mmoja mmoja.

Tazama jinsi kura zilivyopigwa kwa kila muwakilishi na kujua nchi gani ilimpigia kura muwakilishi yupi

votes2

Angola: Koketso
Botswana: Hakeem
Ghana: Feza
Kenya: Hakeem
Ethiopia: Dillish
Malawi: Hakeem
Namibia: Dillish
Nigeria: Dillish
South Africa: Koketso
Sierra Leone: Feza
Tanzania: Feza
Uganda: LK4
Zambia: Hakeem
Zimbabwe: Hakeem
Rest of Africa: Hakeem

Total: Hakeem = 6; Feza = 3; Dillish =3, Koketso = 2, LK4 = 1. (Total: 15 Votes)

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents