Burudani

Big Brother Africa: Hakeem wa Zimbabwe amwandikia ‘Love letter’ Cleo wa Zambia!

Ni mchezo uliojaa ucheshi, furaha, majonzi, karaha, usaliti na mapenzi kwa washiriki 24 (waliobaki) wanaoziwakilisha nchi 14 za bara la Africa kushindania $300,000 zitakazokabidhiwa kwa mshindi mmoja tu atakayepatikana siku ya 91 ya msimu wa 8 wa reality show hiyo ‘The Chase’.

Hakeem & Cleo

Ni mengi yameshajitokeza katika wiki mbili toka shindano lianze (June 26) na washiriki wanne wameshachapa lapa kutoka kwenye jumba hilo na wawili wengine watafungasha virago vyao kesho (June 16) ikiwa ni siku ya eviction ya wiki hii.

Tumeshaziona couple kadhaa zilizoanzisha mahusiano yao mjengoni hapo na kila mmoja anajaribu kufanya kitu cha kumthibitishia mapenzi kwa mwenzie. Hakeem muwaklilishi wa Zimbabwe ni mmoja wao, yeye leo ameamua kumuandikia ‘love letter’ kipenzi chake Cleo au maarufu kama ‘Ice Princess’ katika ulimwengu wa muziki kutoka Lusaka Zambia.

Kama ujuavyo katika mapenzi hata maneno matatu tu yanaweza kubadili usiku kuwa mchana (katika fikra za kimapenzi) hivyo ilikuwa ni barua yenye mistari michache tu inayoonekana kubeba hisia nzito za Hakeem juu yake.

letter-2
Kabla ya uamuzi wa kumuandikia barua Cleo, usiku wa jana Hakeem aliapa kutojihusisha tena na Cleo baada ya Maria kumwambia kuwa Cleo hataki kuishi na Hakeem nyumba moja, hivyo akamuelezea Maria hawezi kuendelea kuwa na msichana ambaye hampendi (akimaanisha Cleo).

Lakini asubuhi ya leo Jumamosi inavyoonekana moyo wa Hakeem uligundua kuwa mwili ulitikisa tu kiberiti, na kuamua kubadili mawazo kisha kumwandikia barua tamu Cleo tena tamu ya herufi kubwa.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents