Burudani

Big Brother Africa: Nando wa Tanzania yuko ‘desperate’ kuchorwa Tattoo, amuomba Biggie amletee mtu wa kumchora mjengoni!

Ni muda umepita hatujasikia story kuhusu wawakilishi wa Tanzania katika Big Brother toka Feza aponee katika tundu la sindano kuiaga $300,000. Lakini kipenzi cha kinadada kijana mtanashati na ‘handsome’ Nando ameibuka na lake baada ya kuanza kuonesha hitaji la kuondoka South Afrika akiwa na kumbukumbu ya mchoro katika mwili wake (Tattoo).

Nando
Wakati wenzake mjengoni wanakimbizana na mapenzi yeye mapenzi yake hivi sasa ni juu ya mwili wake kupata mchoro ‘Tatoo’. Akiwa katika Diary Session Nando alimwomba Big Brother amletee mtu wa kumchora Tattoo mjengoni. Baada ya ukimya bila kumwona mchora Tattoo akija mjengoni, Nando akiwa katika diary session nyingine alimkumbushia tena Big Brother juu ya ombi lake la kuletewa mtu wa kumchora Tattoo.

Well, inavyoonekana ugonjwa wa Tattoo baada ya kukosa tiba ya haraka kwa mgonjwa wa kwanza (Nando) hatimaye virusi vikaanza kuenea katika nyumba ya diamond na kumpata mshiriki mwingine wa Botswana Motamma ambaye alimuunga mkono Nando baada ya kumwomba na yeye Big Brother amfanyie favor ya kumletea mtu wa kumchora Tattoo mjengoni hapo.

Siku Nando akirejea Tanzania iwe na kitita cha $300,000 au laa ukiona mwili wake una Tattoo basi ujue kampeni yake na Motamma ya kuomba kuletewa mchora Tattoo mjengoni ilifanikiwa.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents