Soka saa 24!

Bingwa wa Primier League kujulikana kesho, Manchester City yakutana na vibonde, Liverpool kazi wanayo mbele ya Wolves 

Ligi kuu nchini Uingereza inafikia patamu hapo kesho ambapo iwe jua, iwe mvua lazima bingwa apatikane kati ya Liverpool ama Manchester City.

Image may contain: 2 people, people playing sports and outdoor

Mpaka sasa kila timu imesaliwa na mechi moja kwa timu zote zinazoshiriki Primier League na hakuna aliyena kiporo kutokana na ushiriki wao wa kimataifa UEFA Champions League.

Bingwa mtetezi Manchester City ameshacheza jumla ya michezo 37 katika ligi hiyo yenye timu 20 ikisaliwa na mmoja tu kufikisha idadi ya 38 ambao ni wa hapo kesho dhidi ya Brighton FC inayoshika nafasi ya nne kutoka mkiani huku ikiwa imejikusanyia pointi 95.

Kunako Anfield mpinzani wa City ambaye ni Liverpool mpaka sasa imecheza michezo yake 37 ikiwa imejikusanyia alama 94 ikizidiwa pointi moja tu na Man City, atashuka uwanjani kuvaana na moja kati ya timu kali zaidi inapokutana na wakubwa Wolves.

No photo description available.

Kutokana na utofauti huo wa pointi moja pekee, hivyo kila timu inayonafasi ya kutawazwa kuwa mabingwa wa ligi hiyo kwa msimu wa mwaka 2018/19.

Related Articles

Back to top button
Bongo5

FREE
VIEW