Michezo

Bondia Francis Cheka awa mtoro shuleni

Bondia Francis ‘SMG’ Cheka, amedaiwa kuingia darasani siku moja tu tangu aliposajiliwa kama mwanafunzi mpya wa Chuo cha St Joseph cha mjini Morogoro Septemba mwaka jana.

Francis Cheka mashine

Akizungumza na MWANANCHI, mwalimu wa Cheka aitwaye Mkisi amesema Cheka ameomba kuendelea na masomo baada ya kutoonekana darasani kwa miezi kadhaa bila taarifa yoyote, na kubainisha kuwa hawawezi kumruhusu kuingia muhula wa pili.

Cheka alipewa ufadhili wa masomo chuoni hapo mwaka jana mara baada ya kutwaa ubingwa wa dunia wa WBF Agosti 30, baada ya kumpiga Phil Williams wa Marekani katika pambano lililofanyika jijini Dar es Salaam.

Mkisi amesema kuwa bondia huyo amekosa vipindi kwa muda mrefu hivyo hawezi kuingia muhula mwingine, kwakuwa atakosa vitu vingi hivyo anapaswa kujisajili kama mwanafunzi wa muhula mpya utakaoanza Machi 24.

“Cheka aliingia darasani siku moja na ‘kupotea’ hata hivyo hivi karibuni alikuja na kutuambia anataka kuendelea na shule ingawa hatuwezi kumuendelezea programu yake ya awali,” alisema Mkisi.

Source:Mwananchi

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents