Habari

Fahamu jinsi ya kufanya kazi kwa wema na bosi usiyempenda

Ikiwa ni kutokana na hulka tofauti au tabia tofauti, mtizamo tofauti, mawazo tofauti ama uthamani tofauti wa maisha ikihusisha bosi, msimamizi wako hata meneja, kama unamchukia, kwenda kazini lazima utakuwa ni mzigo mzito kwako. Lakini unaweza kubadili unavyowaza kulingana na mtizamo wako. Hebu tazama mambo haya yanayoweza kukusaidia kuondoa mtizamo hasi kwa bosi wako au meneja wako.

boss
Huwezi kumbadilisha bosi wako tabia, igiza mpaka mambo yaende

Fanya “kama unapenda”

Kuigiza ni jambo linaloweza kukusaidia kuondokana na mikwaruzo isiyohitajika. Kama unamchukia Bosi wako au meneja wako kupambana naye kunaongeza matatizo zaidi na wewe kuwa katika mazingira magumu zaidi. Inamaanisha tabia za kuigiza kana kwamba hakuna tatizo itakusaidia na kukuepusha kwenye mazingira magumu, huwezi kumbadilisha bosi wako tabia, igiza mpaka mambo yaende. Kutafuta kazi nyingine inaweza kuwa sio suluhisho, kama ni vigumu kumpenda, onyesha tabasamu, mheshimu  na kufanya siku yako iishe bila mikwaruzano.

Wekeza nje ya Ofisi

Ingawa itakuwa mbaya sana kumzungumzia bosi wako na wafanyakazi wengine katika kazi, hakikisha matatizo yako ya kiofisi unatafuta mtu unayemwamini nje ya kazi ambaye anaweza kukusaidia na kukupa ushauri .Usionyeshe hasira zako kwa kuandika vibaya labda kwenye mitandao ya jamii, huko ataona. kama una uchungu na hasira rafiki wa karibu au watu wa familia yako wanaweza kukusaidia au mwone mwanasaikologia aliye karibu nawe.

Boresha afya yako zaidi

Kufanya kazi na bosi mkorofi inawezekana ni fursa ya wewe kujitamua na kujua zaidi kuhusu hasira zako, kustahimili mambo magumu au watu wakorofi jinsi unavyojifunza kuishi na watu wakorofi ndivyo unaongeza ujuzi wa kupambana na hali kama hizo zinapokuja siku za usoni. Vilevile inakusaidia kujua ni mbinu gani utumie unapowasiliana naye au kuongea naye bila maudhi na kufanya kazi yako iendelee vizuri.

Tizama Zaidi Utendaji wako wa kazi

Ukizingatia zaidi utendaji wako wa kazi kuliko namna ambavyo bosi anakusumbua na kukukwaza inaongeza mtizamo chanya katika uhusiano wenu. hakikisha kila siku unafanya majukumu yako na kuyamaliza ili usiingie sana kwenye tofauti zenu. Bosi atakapoona unatazama kazi zaidi naye taratibu ataanza kukutizama kikazi zaidi na kuachana na mambo yenu binafsi.

Awali Mwaisanila

A Personal Career Development specialist, passionate about empowering emerging generations of student, graduates and working class.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents