Michezo

Bondia wa Marekani aukimbia ulingo sekunde ya kwanza baada ya kugongwa kengele ya kuanza kwa pambano (+video)

Mwanamasumbwi raia wa Marekani, Curtis Harper ameushangaza umati wa watu waliyouzuria pambano lake dhidi ya Efe Ajagba kwa kutoka ulingoni sekunde ya kwanza tu baada ya kugongwa kwa kengele iliyoashiria kuanza kwa pigano hilo.

Bondia huyo wa uzito wa juu duniani amejikuta akipoteza pambano hilo kirahisi kabisa na kumfanya mpizani wake, Efe Ajagba raia wa Nigeria kutangaziwa ushindi huku mamia ya watu waliyohudhuria pambano hilo wa kilalamikia kitendo hicho.

Inaelezwa kuwa Harper  mwenye umri wa miaka 30 aliamua kutoka na kuondoka zake kutokana na masawala ya maslahi.

Kocha wa bondia huyo, Nate Campbell amesema kuwa kitendo hicho kimemuabisha yeye mwenyewe na kumshushia heshima mkewe, mashabiki pamoja na yeye kama mwalimu.

Mwandishi wa habari anayefanyia kazi Premier Boxing Champions amesema kuwa Harper alimuambia ameamua kundoka ndani ya ulingo kwa sababu ya fedha.

“Aliamua kuondoka ndani ya ulingo kutokana hajalipwa kiasi cha kutosha ambacho kingemfanya kupigana na kufanya hivyo ni kwa sababu ya kutaka heshima,” alisema mwandishi huyo.

Wakala, Leon Margules amewaambia waandishi wa habari kuwa hakuwa na wazo kuwa Harper anampango wa kuondoka ulingoni na pambano mpambanaji huyo hatopata malipo yake.

Related Articles

7 Comments

  1. Jifunzeni kufungua links kabla ya comment waungwana mkiendekeza hivyo na comment zenu zisokuwa na kichwa wala miguu mtajiona wajinga kabisa hebu funguon na musome alafu angalia coment yako inaendana na tukio lilivyo au mupo wengi wakukurupuka kama yuleeeee

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents