Michezo

Bondia wa Marekani, Patrick Day mahututi baada ya kuchezea kipigo, atolewa ulingoni kwa machela

Bondia wa Marekani Patrick Day yupo mahututi baada ya kupigwa akiwa ulingoni katika roundi ya 10 na mpinzani wake Charles Conwell.

Image result for Patrick Day
Patrick mwenye miaka 27 alipata majeraha makubwa katika ubongo hali iliyopelekea kupoteza fahamu mpaka sasa ambapo amelazwa katika hospitali ya Northwestern Memorial nchini Marekani.

Baada ya pambano hilo lililokomea roundi ya 10, Patrick alibebwa kwa machela kutolewa ulingoni huku akiwa amepoteza fahamu na kuwahishwa hospitali.

Image result for Patrick Day

Patrick Day akipigwa ngumi ya kidevu

Vyombo vya habari nchini Marekani vimeripoti kuwa, Patrick Day amepata ‘coma’ hajaamka mpaka sasa tangu ilipigwa ulingoni usiku wa Jumamosi kwa KO na Charles Conwell pambano lilifanyika Chicago.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents