BOOMPLAY MUSIC YASHINDA TUZO YA ‘BEST AFRICAN APP’ KWENYE TUZO ZA THE APPSAFRICA INNOVATION 2017

Boomplay Music, jukwaa la kupakua na kusikiliza muziki linalokua kwa kasi zaidi Afrika, Iimeendelea kuimarisha mchango wake kwenye mfumo wa usambazaji muziki, hasa baada ya mchango wake kutambuliwa na jopo huru la wataalamu wa tasnia ya teknolojia kwenye tuzo za AppsAfrica. AppsAfrica ni tovuti inayojihusisha na habari za kitekinolojia na utoaji wa ushauri wa kitaalamu unaoangazia ufahamu wa maswala ya simu, tekinolojia na ubunifu.

Boomplay Music imeshinda tuzo ya App Bora Afrika (Best African App), kutokana na upekee na urahisi wa kuitumia. App ya Boomplay Music inakuwezesha kupata nyimbo zaidi ya milioni , video na habari za burudani. Tuzo hiyo ilikabidhiwa kwenye sherehe za utoaji wa tuzo hizo zilizofanyika nchini Afrika Kusini mjini Cape Town mnamo tarehe 6, Novemba 2017. Katika kipengele hicho tuzo hiyo ilishindaniwa pia na Carter – Afrika kusini, Asorbia – Ghana, Truecaller Africa and FeastFox – Afrika Kusini. Boomplay Music ilifanikiwa kuwabwaga washindani wake na kufanikiwa kuwa app ya kwanza ya kupakua na kusikiliza muziki kufanikiwa kushinda tunzo hiyo.

Hadi kufikia Oktoba, 2017, watumiaji wa Boomplay Music wameongezeka hadi kufikia milioni 15, ikilinganishwa na milioni 6 mwishoni mwa mwaka 2016. Kwa sasa watumiaji wa mara kwa mara wameongezeka kufikia milioni 9, ikilinganishwa na milioni 2 mwishoni mwa mwaka 2016. Kulingana na maelezo ya mkurugenzi mkuu wa Boomplay Music, Bwana Joe He, zaidi ya watumiaji milioni 2 kwa sasa wanatumia app kusikiliza muziki, kutazama video na kusoma habari kila siku.
Boomplay Music app imeshinda tuzo kutokana na urahisi wakuitumia, mwonekano mzuri na ubunifu, haswa kwa namna inavyorahisisha upatikanaji wa muziki kwa mamilioni ya waafrika, na kuchochea wanunuzi wa muziki kuongezeka, wakati ikisaidia kupunguza uharamia kupitia mikakati mizuri ya kibiashara, kuhakikisha hati miliki zinalindwa kwa jitihada zote. Boomplay inaamini kwamba wamiliki wa kazi za sanaa ya muziki wanaweza kufaidika na mauzo ya kazi zao.

Alipopewa nafasi ya kuzungumza kuhusiana na tuzo hiyo, Mkurugenzi Mkuu wa Boomplay Music, Bwana Joe He alisema: “Kunyakua tuzo ya Best African App kunaonyesha kufanikiwa kwa jitihada zetu za kujenga mfumo bora na endelevu kwa wamiliki wa kazi za sanaa ya muziki, wakati huo huo tukihakikisha kazi za sanaa ya muziki zinawafikia watumiaji kwa urahisi zaidi. Kwa kipindi kifupi tu cha miaka miwili mafanikio tuliyoyapata ni ya kuvutia. Kwa niaba ya Boomplay Music, tuzo hii imetupa nguvu na tutaendelea kuhakikisha fikra zetu zinaangazia namna ya kukabiliana na changamoto za matumizi ya kazi za sanaa ya muziki zilizopo kwenye mfumo wa kidijitali kwa njia rahisi na za kibunifu zaidi kwa msaada wa tekinolojia”.
Boomplay Music app kwa sasa inapatikana kwa vifaa vyote vyenye mfumo wa android kupitia Google Play Store na itapatikana kwa watumiaji wa iOs ifikapo mwaka 2018.

Related Articles

Back to top button
Close
Bongo5

FREE
VIEW