Boss mpya Yanga aweka mezani kitita cha Milioni 10 kununua pointi 3 mbele ya Ndanda FC (+video) 

Mdhamini mpya wa klabu ya Yanga, ambaye ni msambazaji wa jezi zao, GSM ameweka mezani kitita cha shilingi milioni 10 ili kuhakikisha timu hiyo inachomoza na ushindi wa alama tatu dhidi ya Ndanda FC mchezo wa ligi kuu Tanzania Bara.

Mabingwa hao watetezi hii leo watashuka uwanjani huko Mtwara kucheza mchezo huo wa ligi dhidi ya wenyeji wao timu ya Ndanda FC.

Kupitia afisa mhamasishaji wa Dar es Salaam Young Africa, Antonio Nugaz amesisitiza kuwa mdhamini wao ametoa kiasi hicho cha pesa ili kununua pointi tatu hii leo.

”Mdhamini wetu ambaye ni Msambazaji wa jezi zetu kupitia Brand Chapa @gsmtanzania GSM leo Ijumaa kuelekea mchezo wetu dhidi ya Ndanda fc ya Mtwara ameweka mezani tena ahadi ya pesa taslimu shilingi milioni kumi {10,000,000} kwa ajili ya hamasa ya kupata point tatu muhimu.
#Shukran kwa GSM kwa kuweza kuleta motisha.” – Maneno yaliyoandikwa na mtandao wa klabu hiyo ya Jangwani.

Related Articles

Back to top button
Close
Bongo5

FREE
VIEW