Picha
Breaking: Mbunge wa Chambani (CUF) Salim Hemed Khamis afariki dunia
Mbunge wa Chambani (CUF),Salim Hemed Khamis amefariki dunia leo baada ya kulazwa jana kwenye hospitali ya taifa ya Muhimbili.
Jana mbunge huyo alihudhuria vikao vya kamati za bunge lakini wakati akiendelea na kikao kwenye kamati alianguka ghafla kutokana na kujisikia vibaya na kupelekwa hospitali ya Muhimbili na wabunge wenzake.
Inadaiwa kuwa hali yake asubuhi ya leo iliendelea kuwa mbaya na majira ya saa sita na kitu mchana ikatolewa taarifa kuwa ameshafariki dunia. Sababu za kifo cha mbunge huyo inadaiwa kuwa ni shinikizo la damu.
Khamis aliyezaliwa September 20, 1951 amekuwa mbunge wa jimbo la Chambani tangu mwaka 2005.