Afya

Breaking: Mgonjwa wa kwanza wa Corona Tanzania apatikana , Waziri wa Afya athibitisha – Video

Breaking: Mgonjwa wa kwanza wa Corona Tanzania apatikana , Waziri wa Afya athibitisha - Video

Mwanamke Mtanzania mwenye umri wa miaka 46 ambaye aliwasili nchini akitokea Ubelgiji kwa Ndege ya Shirika la ndege la Rwanda katika Uwanja wa Ndege wa KIA, mkoani Kilimanjaro amethibitika kuwa na maambukizi ya virusi vya Corona.

Kwa mujibu wa Waziri wa Afya Ummy Mwalimu, mwanamke huyo aliwasili nchini Machi 15 akitokea nchini Ubeligiji na kufanyiwa uchunguzi katika Uwanja huo na kuonekana kutokuwa na homa lakini baadaye alijisikia vibaya na kwenda katika Hospitali ya Mount Meru mjini Arusha na kuchukuliwa vipimo vilivyothibitisha kuwa na maambukizi ya virusi vya Corona yaani COVID -19.

Waziri Ummy amesema, kwa sasa Mwanamke huyo anapatiwa matibabu na anaendelea vizuri na kuwasihi Watanzania wasiwe na hofu na badala yake wafuate maelekezo na elimu inayotolewa nchini ili kujikinga na maambukizi hayo.

https://www.instagram.com/p/B9y0d05hfRd/

https://www.instagram.com/p/B9y0wnKBEkT/

 

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents