Habari

Busta Rhymes ashitakiwa na studio aliyorekodi kazi bila kulipa hata senti toka mwaka 2011

Kwa uzoefu wa hapa Tanzania studio nyingi za muziki hazi charge wasanii kwa masaa (sio zote) bali kwa kazi anayotaka kufanya msanii, kitu ambacho wakati mwingine kinasababisha baadhi ya wasanii kushinda katika baadhi ya studio hata kama hawana kazi maalum wanayofanya muda huo.

busta_rhymes

Hii ni tofauti kwa studio za nchi zilizoendelea ambapo wanacharge msanii kwa masaa atakayotumia hapo studio, hivyo kama msanii alipewa session ya masaa matatu na akazidisha atatakiwa kulipia muda wote uliozidi.

Hili limemkuta rapper Buster Rhymes ambaye style yake ya kurap huitaji nguvu ya ziada na siyo ya (spaghetti), ambaye amejikuta akishitakiwa na Paramount Recording Studios kwa kutumia studio time iliyotokana na recording sessions kadhaa alizopewa mwaka 2011 ambazo hakulipa hata senti.

Madai ya studio ya PRS ni kuwa Busta Rhymes alitumia masaa yapatayo 375 kama recording sessions kwa mwaka 2011-2012 na hajawahi kulipia hata senti, hivyo studio hiyo imemfungulia mashitaka kudai malipo yanayofikia $70,300.

Nyaraka za mashitaka hayo zimeonesha muda ambao Busta alikuwa akifanya kazi katika studio za PRS,

December 5th, 2011 — Busta aliingia studio saa 9 jioni na kuondoka saa 1 asubuhi (siku iliyofuata)
January 15th, 2012 – Aliingia saa 1 jioni na kutoka saa 9 asubuhi
January 18th, 2012 – aliingia saa 9 alasiri na kutoka saa 12 asubuhi
February 12th, 2012 – aliingia saa 4 usiku na kutoka saa 12 asubuhi

Kwa Mujibu wa mtandao wa TMZ Busta Rhymes hakupokea simu alipotafutwa kutoa maelezo yake.

Kama studio zote za bongo zingetumia mfumo huu ingepunguza sana usumbufu kwa maproducer kuzungukwa na wasanii wanaokuwa hawana kazi maalumu lakini wanashinda hata siku nzima studio wakipiga story.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents