Michezo

‘Chelsea wamezeeka’ Giggs.

 


Winga wa Manchester United,Ryan Giggs amesema klabu ya Chelsea imezeeka kuliko yake.

Kiungo mshambuliaji ameyasema hayo ikwa ni siku moja baada ya Manchester United kuichapa Chelsea mabao 3-1 kwenye mchezo wa ngao ya jamii.

Giggs alisema ‘Nafikiri tuliweza mpira,Chelsea ni timu nzuri lakini jinsi tulivyocheza tuliwafanya waonekane wazee sana’.

Nivizuri kwakuwa tumeweza kushinda,na hii ndio inaonyesha tofauti ya timu yetu na yao, Kazi kubwa ya michuano ya maandalizi ya ligi ni kumaliza salama mkiwa mnashinda na kutoka bila kuwa na majeruhi.

Tunajiamini na maandalizi yamemalizika sasa tunaangalia ligi tukiwa na sura nyingine,Manchester United watajitupa kumenyana na Newcastle leo.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents