Michezo

Chelsea yakubali yaishe kwa Diego Costa

Mabingwa watetezi wa Ligi Kuu nchini Uingereza, klabu ya Chelsea imekubali yaishe juu ya uhamisho wa mchezaji wake, Diego Costa kujiunga na Atletico Madrid ya Hispania.

Costa ambaye amejiunga na Chelsea akitokea Atletico mwaka 2014 kwa dadu la paundi milioni 32, anatarajiwa kufanyiwa vipimo vya Afya siku za hivi karibuni.

imesema kuwa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 28 ambaye aliondoka katika klabu hiyo na kujiunga na Chelsea 2014 atafanyiwa ukaguzi wa kimatibabu siku chache zijazo.

Diego Costa mwenye umri wa miaka 28, hajajiunga na kikosi cha Chelsea msimu huku akitumia muda mwingi mapumzikoni nchini Brazili.

Chelsea na Atletico zinatarajia kukutana katika mchezo wa klabu bingwa barani Ulaya siku ya Jumatano.

Mshambuliaji huyo raia wa Brazili amefunga jumla ya mabao 58 katika michezo 120.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents