Technology

China yaongoza kwa kuwa na computer yenye kasi zaidi duniani, ina kasi zaidi ya PC za kawaida milioni 338 zikiwa pamoja

China imetengeneza computer yenye kasi zaidi duniani – mara mbili ya ile iliyotengenezwa na Marekani. Computer hiyo ina kasi zaidi kuliko PC za kawaida milioni 338 zikiwekwa pamoja.

article-2343265-1A5DBA7B000005DC-507_634x421

The Tianhe-2, ambayo maana yake ni Milky Way 2, iliundwa na chuo kikuu cha technolojia ya ulinzi cha nchini humo katika jiji la Changsha.

Taarifa hiyo ilichapishwa kwenye ripoti ya TOP500 – ripoti ya kila mwaka inayoorodhesha supercomputer zenye kasi zaidi duniani.

Kwa mujibu wa orodha hiyo, Marekani imechukua nafasi ya pili, tatu, tano, sita na ya nane.

K computer ya Japan imekamata nafasi ya nne huku Juqueen na SuperMuc za Ujerumani zikikamata nafasi ya saba na ya tisa.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents