Michezo

Chirwa amalizana na wadhamini wa ligi kuu

Mshambulizi wa Yanga, Obrey Chirwa amekabidhiwa Tsh Milioni 1 na Afisa Udhamini wa Matukio wa Vodacom Tanzania, Ibrahim Kaude mapema leo wakati timu yake ikifanya mazoezi kujiandaa na mechi dhidi ya Mbeya City Jumapili hii. Bodi ya Ligi iliwakilishwa na Meneja Fedha, Ibrahim Mwayela na Joel Balisdya. Kaimu Afisa Habari wa Yanga, “Chicharito” ameishukuru Vodacom kwa kuwapa wachezaji motisha, zaidi tizama video hii.

Wadhamini wa Ligi Kuu soka Tanzania Bara kampuni ya Vodacom wamemalizana na mshambuliaji wa Yanga SC, Obrey Chirwa kwa kumkabidhi kitita cha shilingi milioni moja ikiwa ni zawadi ya kuwa mchezaji bora wa mwezi Oktoba wa VPL.

Afisa Udhamini wa Matukio wa Vodacom Tanzania, Ibrahim Kaude mapema leo wakati timu ya Yanga SC ikifanya mazoezi kujiandaa na mechi dhidi ya Mbeya City Jumapili hii. Bodi ya Ligi iliwakilishwa na Meneja Fedha, Ibrahim Mwayela na Joel Balisdya. Kaimu Afisa Habari wa klabu hiyo, “Chicharito” amemkabidhi Chirwa kiasi hicho cha fedha.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents